Tuzo za Grammy zahairishwa

0
11

Tuzo za Grammy za mwaka 2021 hazitafanyika tena mwezi huu huko Los Angeles, California, na badala yake zitatangazwa mwezi Machi kwa sababu ya kuongezeka kwa visa vya virusi vya corona na vifo.

 

Waandaji wa tuzo hizo walisema Jumanne wiki hii kuwa onyesho hilo la kila mwaka litasogezwa mbele kutoka tarehe yake ya awali ya Januari 31 hadi tarehe isiyojulikana mwezi Machi.

 

Tuzo hizo za Grammy zitafanyika Los Angeles katika Kituo cha Staples, Kaunti ya Los Angeles, ambako ndiko kitovu cha ugonjwa huo  huko California, ambako umeua zaidi ya watu 10,000.

 

Mwanamuziki nyota wa Marekani, Beyonce ndiye anayeongoza katika tuzo hizo mwaka huu akiwa na ameteuliwa katika vipengere tisa.

LEAVE A REPLY