Tunda ndani ya bifu zito na Aunty Ezekiel kisa pesa ya Pombe

0
380

Muigizaji wa Bongo Movie, Aunty Ezekiel amerushiana maneno makali na video vixen Bongo, Tunda kisa ela ya pombe kwenye mtandao wa kijamii.

Hali hiyo imetokea jana baada ya Aunty Ezekiel kwenda kwenye ukurasa wa Instagram wa Tunda na kumdai pesa yake kiasi cha laki moja baada ya Tunda kukopa pombe aina ya Belaire.

Aunty Ezekiel ameanza kwa kuandika “Tunda naomba pesa zangu za pombe please mm mwenyee napenda kuwa boss ila siuwezi ndiyo mana nauza pombe please mm siyo dizain yenu naomba usicheze na pesa yangu’.

Baada ya Aunty kumuandikia vile inaelekea Tunda hakupenda kabisa kwani mara moja alianza kutokwa na povu kueleza kuwa alimpa pesa Mose Iyobo na kumtuhumu kwa kuitumia pesa ile.

Tunda nae akajibu “Uzee unakujia vibaya we we Bibi Mdashi na Una lako jingine nje ya pombe jibu ni lile lile ongea na Ben-ten wako akueleze pesa alipopeleka”.

LEAVE A REPLY