Tunda aweka hadharani mapenzi yake na Whozu

0
864

Video vixen wa muziki wa Bongo Fleva, Tunda amethibitisha kutoka kimapenzi na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Whozu ambaye kwasasa anatamba na wimbo ‘Doko’.

Tunda amefunguka hayo wakati wa sherehe ya siku yake ya kuzaliwa iliyofanyika katika hoteli ya Hayatt jijini Dar es Salaam na kuwathibitishia baadhi ya watu waliohudhuria sherehe hiyo katika hoteli hiyo maarufu jijini.

Pia Tunda amesema kuwa yeye na Whozu ni watu waliokuwa wanafahamiana tangu shule ya msingi, pia nyumbani kwao ni majirani huko Moshi mkoani Kilimanjaro.

Taarifa za wawili hao kuanza kuenea kuwa wanatoka kimapenzi zilianza kusambaa katika mitandao ya kijamii kwa muda mrefu lakini walikuwa wanakataa mpaka walipothibitisha hilo mbele za mashabiki wao.

Aidha Tunda amesema anatamani kufika mbali na mpenzi wake huyo, sababu anampenda sana anatamani adumu naye, waonane na wawe na familia.

Penzi la Tunda na Whozu limekuja kwa kasi sana na limekuwa likizungumziwa na watu wengi sana kupitia mitandao ya kijamii. Mrembo huyo amewahi kuwa kwenye mahusiano na wasanii na watu wengine maarufu kama Yound Dee na Casto Dickson.

LEAVE A REPLY