Tunda amtupia dongo Hamisa baada ya video yake na Diamond kuvuja

0
253

Video queen Bongo, Tunda Sebastian amemtupia dongo Hamisa Mobetto baada ya video zake za chumbani na Diamond kuvuja mtandaoni.

Jana Diamond na Hamisa walizua gumzo baada ya kuonekana pamoja chumbani wakiwa wanakumbatiana kwenye mahaba mazito jambo lililozua gumzo kuwa wamerudiana.

Lakini muda mfupi baada ya Hamisa kuonekana na Diamond video zilizomuonyesha Diamond na demu wa kizungu wakila Madenda nazo zilivuja mtandaoni jambo lililowachanganya watu wengi kuona Diamond na wanawake wawili tofauti katika usiku mmoja.

Tunda na Hamisa wameshawahi kuwa na bifu siku za nyuma huku ikiaminika kuwa walikuwa wanamgombania Diamond kwani wote wawili wameshahusishwa kuwa na Mahusiano na Diamond.

Tunda ameibuka na kumpa Dongo Zito Hamisa baada ya video zake na Diamond kusambaa mtandaoni ambapo amedai kuwa anamuonea huruma Hamisa maana amedhalilishwa na mwanaume ambaye ni wazi kabisa kuwa hamtaki.

LEAVE A REPLY