Tunda afunguka mipango ya ndoa yake

0
215

Video vixen Bongo, Tunda ameibuka na kudai kuwa anaolewa hivi karibuni na mwanaume ambaye sio staa kwani ameshavalishwa pete ya uchumba hivyo ndoa ipo karibu.

Kauli ya mrembo huyo imekuja baada ya mashabiki wake kuanza kuanza kuhoji pete yake ya uchumba aliyekuwa nayo.

Tunda amesema pete ambayo inaonekana kidoleni mwake siyo feki kama baadhi ya watu wanavyodhani na watu wajue kwamba atakayemuoa ni mwanaume wa kawaida na siyo staa.

Pia amesema kuwa anaolewa hivi karibuni na anafurahi kuwa anaolewa na mtu anayempenda na anayejielewa na sio kama drama za wale watu wengine waliopita, hvyo ameamua kujituliza kabisa.

Miezi michache iliyopita mrembo huyo alikuwa kwenye mapenzi moto moto na mtangaji wa kituo cha Clouds tv, Castro Dickson ambapo kwasasa wawili hao wameachana na kila mmoja kuanzisha mapenzi na mtu mwingine.

LEAVE A REPLY