Tunda afunguka mahusiano yake

0
82

Video vixen maarufu Bongo Anastasia Sebastian maarufu kama Tunda amefunguka na Kusema tofauti na watu wengi wanavyomfikiria yeye anaweza sana kudumu na mwanaume kwenye mahusiano.

Tunda amewajia juu na kuwashangaa watu wanaomuona yeye  hawezi kudumu na mwanaume mmoja, lakini ni kwa sababu hapendi kufanyiwa ujinga kisha kunyamaza kama walivyo wanawake wengine.

Tunda amesema kuwa sasa hivi wanaume wengi wanapenda kuwachezea wanawake kwa sababu wanawajua ni dhaifu, lakini wangejitambua thamani yao wala wasingekubali kupelekeshwa na wanaume.

Tunda amedaiwa kumwaga mpenzi wake wa Miezi kadhaa Casto Dickson na kuanzisha Mahusiano na Jamaa mwingine lakini juzi Tena ameonekana na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

LEAVE A REPLY