Tunajianda na mazoezi ya ligi kuu: Salum Mayanga

0
150

Kocha mkuu wa Mtibwa Sugar, Salum Mayanga amesema kwa sasa wanajianda na ligi kuu Tanzania Bara msimu ujao licha ya kupata mapungufu katika sehemu mbalimbali kufuatiwa na baadhi ya wachezaji kuihama timu hiyo.

Mtibwa Sugar imefanya usajili baada ya kuondokewa na wachezaji wao watatu ambao ni  Vicent Andrea ambaye amejiunga na Yanga, Mohamed Yassin na Shiva Kichuya waliojiunga na Simba SC.

  Wachezaji waliosajiliwa na Mtibwa Sugar ni Haruna Chanongo, Kasiani Mponela na Rashid Madawa ambao wanategemea kuleta mabadiliko ndani ya kikosi hiko.
 Mtibwa Sugar itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mbeya City katika uwanja wa Jamhuri, mkoani Morogoro kuwajaribu wachezaji wao kabla ya kuanza kwa ligi kuu ya Tanzania Bara.

LEAVE A REPLY