Tshishimbi awatoa hofu mashabiki wa Yanga

0
195

Kiungo wa Yanga, Papy Tshishimbi amewaambia mashabiki wa timu hiyo kuwa baada ya kutolewa kwenye kombe la Mapinduzi nguvu zote wamehamishia kwenye ligi kuu Tanzania Bara.

Yanga iliondolewa na URA ya Uganda katika michuano hiyo, kwa kufungwa kwa njia ya penalti 5-4 baada ya dakika 90 kumalizika kwa suluhu.

 Jana Jumapili Yanga ilianza maandalizi ya ligi kuu katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam chini ya Kocha Mkuu George Lwandamina.

Siku ya Jumatano Yanga itashuka dimbani kucheza dhidi ya Mwadui FC katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Kiungo alitoa kauli hiyo kupitia moja ya akaunti zake za kijamii akiwataka mashabiki wa timu hiyo kutokata tamaa baada ya kulikosa Kombe la Mapinduzi na badala yake kuelekeza nguvu katika ligi kuu ili wautetee ubingwa wao.

Tshishimbi alisisitiza kuwa, mapambano yanaendelea licha ya kuondolewa katika michuano hiyo huku akiahidi kufanya vema katika mechi zao zijazo za ligi kuu.

LEAVE A REPLY