Tshishimbi atangazwa mchezaji bora wa mwezi Februari

0
238

Kiungo wa Yanga Papy Kabamba Tshishimbi ametangazwa kuwa mchezaji bora wa Ligi kuu kwa mwezi Februari.

Tshishimbi amefanikiwa kutwaa tuzo hiyo baada ya kuisaidia klabu yake ya Yanga, kuchukua alama 12 zote katika michezo minne iliyopigwa ndani ya mwezi Februari akifunga mabao matatu na kusaidia bao moja.

Tshishimbi amewaacha wapinzani wake kwenye kinyang’anyiro hicho ambao ni kiungo mwenzake wa Yanga Pius Buswita, aliyefunga mabao mawili pamoja na mshambuliaji wa Simba Emmanuel Okwi aliyefunga mabao 4 na kuisaidia Simba kupata alama 10 katika mechi 4.

Nyota huyo raia wa DR Congo atakabidhiwa zawadi zake ikiwemo zawadi kubwa ya shilingi milioni moja kutoka kwa wadhamini wa ligi kuu pamoja na tuzo ambayo imetambulishwa msimu huu na TFF.

LEAVE A REPLY