Tshishimbi aanza mazoezi mepesi

0
202

Kiungo wa Yanga, Kabamba Tshishimbi anatarajia kurudi uwanjani kwenye mechi dhidi ya Mbao Fc baada ya kaanza mazoezi mepesi leo.

Tshishimbi alikuwa nje kwa muda wa wiki moja na nusu akiuguza majeraha ya kifundo cha mguu aliyoyapata wakati timu hiyo ikijiandaa na mechi dhidi ya Mbeya City.

 Yanga imeanza mazoezi yake leo baada ya kumaliza mapumziko ya wiki moja waliyopewa na Kocha Mkuu wa timu hiyo.

Kwa upande wa Daktari Mkuu wa timu hiyo, Edward Bavo amesema kiungo huyo yupo fiti hivi sasa na huenda akawepo kwenye orodha ya wachezaji watakaoivaa Mbao FC.

LEAVE A REPLY