Trump: Tumechoka kuivumilia Korea Kaskazini

0
180

Rais wa Marekani, Donald Trump amesema muda wa uvumilivu wa kimikakati kwa Korea Kaskazini umekamilika sasa.

Katika hotuba ya pamoja na rais wa Korea Kusini Moon Jae, kwenye ikulu ya White house, Trump amesema kwamba vitisho vya Korea Kaskazini vinafaa kupata majibu ya kijasiri.

Hata hivyo, Trump amesema ni muhimu kuwe na ushirikiano katika kugawana mzigo wa kuhakikisha usalama.

Rais wa Korea Kusini amesema kwamba taifa lake litaweka marekebisho ya kiuslama na kujenga msingi dhabiti wa kujikinga.

Rais Moon pia amesema ni muhimu kuendelea na majadiliano na viongozi wa Korea Kaskazini.

Kwengineko, Bwana Moon alisema kuwa ni muhimu kuendelea kujadiliana na viongozi wa Korea Kaskazini.

Moon alisema kuwa swala la Korea Kaskazini linafaa kupewa kipaumbele wakati wa mazungumzo akisisitiza kuwa ni usalama thabiti pekee unaoweza kuleta amani katika eneo zima la Pacific.

Akizungumza katika Ikulu ya Whitehouse, bwana Trump alisema kuwa wakati wa kuvumiliana na utawala Korea Kaskazini umefeli miaka mingi akiongezea: Kwa kweli uvumilivu huo umekwisha.

Kiongozi huyo wa Marekani amesema kuwa serikali yake sasa inafanya kazi na Korea Kusini pamoja na Japan wakiwemo washirika wengine duniani kuchukua hatua kadhaa za kidiplomasia, usalama na kiuchumi ili kuwalinda washirika wake pamoja na raia wa Marekani dhidi ya janga hilo kwa jina Korea Kaskazini.

LEAVE A REPLY