Trump: Nitadhibiti wahamiaji nchini Marekani

0
145

Mgombea urais wa chama cha Rupublican nchini Marekani, Donald Trump amesema kuwa atabuni mfumo ambao utasaidia serikali kudhibiti uhamiaji haramu nchini humo.

Trump amesema kuwa mfumo huo utasaidia kuwatimua watu ambao wanaishi nchini Marekani licha ya muda wa visa zao kumalizika.

Pia alirejelea wito wake wa kujengwa ukuta kati ya mpaka wake na Mexico kuwazuia wahamiaji kutoka nchini Mexico.

LEAVE A REPLY