Trump kuitoa Marekani kwenye mkakati wa mabadiliko ya hali ya hewa?

0
206

Imeripotiwa kuwa rais mteule wa Marekani, Donald Trump ameanza kutafuta njia za haraka za kuiondoa Marekani kwenye makubaliano ya kidunia juu ya namna ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa.

Endapo mpango huo utafanyiwa kazi pindi atakapoapishwa kuwa rais wa nchi hiyo, Marekani itajitenga na nchi nyingine zinazopambana na kuhamasishana kupunguza uzalishaji wa hewa chafu kutoka viwandani ambao kwa kiasi kikubwa umekuwa ukichangia mabadiliko hayo ya hali ya hewa.

Rais huyo anadai wa kuuita mpango huo wa kudhibiti ongezeko la joto duniani kama uongo unaochekesha na ameahidi kujitoa kwenye makubalino ya Paris ambayo yalikuwa yakiungwa mkono kwa nguvu na rais anayeondoka madarakani, Barack Obama.

Kwa mujibu wa mtoa habari aliyetaka jina lake lihifadhiwe amedai kuwa timu ya washauri na wataalamu ya rais mteule inatafuta njia ya mkato ya kujitoa kwenye makubaliano hayo badala ya kufuata njia ya kawaida ambayo inachukua miaka minne.

Hata hivyo Trump anaweza akakabiliwa na changamoto kubwa ndani ya chama chake kwakuwa mtangulizi wake, rais mstaafu George Bush ndiye aliyesaini mkataba wa U.N. Framework Convention on Climate Change (UNFCCC) na pia uliungwa mkono na baraza la seneti.

LEAVE A REPLY