Trump atimiza siku 100 toka awe Rais wa Marekani

0
135

Rais wa Marekani, Donald Trump ameadhimisha siku mia moja toka awe rais wa taifa hilo kwa kutoa hotuba ya kushambulia wanahabari na kutetea mafanikio yake.

Trump amewaaambia wafuasi wake huko Pennsylvania kwamba ameridhika kuwa pamoja nao badala ya kuhudhuria dhifa ya chakula cha jioni na wanahabari ama ‘Correspondents diner’ iliyokuwa ikifanyika katika ikulu ya White House wakati huo.

Akihutubia umati mkubwa katika jimbo la Pennsylvania, Rais Trump amelinganisha na kutofautisha kile ametaja ‘siku mia moja za wanahabari kushindwa na kazi yao.

Pia amesema amekuwa akitimiza ‘ahadi zake kila siku’, hususan kurejesha kazi za viwanda na kumaliza mzozo katika sekta ya makaa ya mawe.

Pennsylvania ni jimbo linalotegemea uchumi wa uchimbaji madini, na lilikuwa muhimu sana katika uchaguzi wa mwaka jana.

Awali maelfu ya watu waliandamana nchini Marekani dhidi ya utawala wa rais Trump na msimamo wake kuhusu mazingira.

LEAVE A REPLY