Trump apingwa vikali ‘Uingereza’ tiara yake kujadiliwa Bungeni ‘leo’

0
207

Kauli ya rais wa Marekani dhidi ya raia kutoka nchi saba za Kiislam ambao amewapiga marufuku imeanza kumtokea puani.

 Baada ya kuzungumzia sana suala la kuwapiga vita waislam na kisha kusaini sheria ya kuwapiga marufuku raia kutoka nchi saba za kiislam kuingia nchini Marekani imeanza kumrudia mwenyewe kwani watu zaidi ya milioni moja wamepinga ziara yake.

Baada ya kuwekwa kwa kura ya maoni mtandaoni juu ya aidha kukubali au kukataa rais huyo wa Marekani kufanya ziara ya kikazi nchini Uingereza, zaidi ya watu milioni moja wamesaini kupinga ziara hiyo.

Waziri mkuu wa Uingereza, Theresa May alitangaza kuwa rais Trump ataitembelea nchi hiyo siku za karibuni kufuatia ziara yake May nchini Marekani.

Hata hivyo ikulu ya waziri mkuu ya Downing Street imekataa kufuta ziara hiyo.

Mbunge wa chama cha Labour, Jeremy Corbyn ametoa maoni yake na kumuomba waziri mkuu, Theresa May kusitisha ziara hiyo kwasababu matokeo ya kusainiwa kwa malalmiko hayo mtandaoni na watu zaidi ya milioni moja inamaanisha kuwa:

‘Donald Trump aruhusiwe kuingia Uingereza kama rais wa Marekani lakini asipewe mwaliko wa dhifa na Malkia kwasababu hiyo itamuaibisha Malkia’.

Dhifa ya kitaifa ni shughuli kubwa ambayo huhitaji mwaliko rasmi wa Malkia na hutofautiana na mialiko mingine ya kawaida ya viongozi wa juu wa mataifa kutembelea Uingereza kwaajili ya shughuli za kikazi.

Kwa kawaida Malkia hupokea hadi wakuu wa nchi wawili tu kwa mwaka kwaajili ya dhifa ya kitaifa.

Aliyeanzisha mchakato wa kura hiyo, Graham Guest, ameliambia shirika la habari la Press Association kuwa endapo Trump atapata mwaliko wa Ikulu hiyo itahalalisha urais wake na atatumia picha atakazopiga na Malkia ili kuchaguliwa tena.

Ziara ya Trump sasa itajadiliwa na bunge la Uingereza siku ya leo na huenda ikulu ya Waziri Mkuu ikatoa taarifa yake baada ya kikao cha Bunge endapo ziara hiyo itaendela kama ilivyopangwa au itafutwa.

LEAVE A REPLY