Trump amualika Kenyatta nchini Marekani

0
100

Serikali ya Kenya imepokea mwaliko kutoka nchini Marekani kuhudhuria katika hafla ya kuwashukuru kwa kuendeleza urafiki itakayofanyika Januari 13, 2018.

Mwaliko huo umekuja ikiwa ni baada ya Kenya kuwa miongoni mwa nchi ambazo hazikupiga Kura ya kupingana na uamuzi wa Rais wa Marekani, Donald Trump kuutambua Jerusalem kuwa Mji Mkuu wa Israeli

Siku moja kabla ya zoezi la upigaji kura, Rais Trump alionya kukata misaada kwa nchi zote ambazo zingepiga kura ya kumpinga

Tanzania ni miongoni mwa nchi 128 ambazo zilipiga kura ya kumpinga Rais Donald Trump huku Kenya ikiwa ni miongoni mwa nchi 9 pekee zilizomuunga mkono.

 

LEAVE A REPLY