Trump ameagiza ukaguzi makini kufanyika mipakani

0
113

Rais wa Marekani, Donald Trump amewaagiza maafisa wa usalama wa mipakani kuwakagua kwa makini watu wanaoingia Marekani.

Kauli hiyo ya Trump inakuja baada ya mahakama ya rufaa kukataa ombi la serikali ya Marekani la kurejesha amri ya kuwazuia wahamiaji ambapo ofisi ya mwanasheria mkuu imepewa nafasi hadi leo kujibu maamuzi hayo.

Trump amesema kuwa mahakama ambayo imezuia hatua hiyo inafanya vigumu kuimarisha usalama katika mipaka ya Marekani na kumshtumu jaji aliyetoa uamuzi huo kwamba analiweka taifa hilo mashakani.

Pia ameongeza kwa kusema kuwa iwapo kutakuwa na tukio lolote jaji huyo na mfumo wake wote wa mahakama utalaumiwa.

Awali mahakama ya kijimbo ilikataa ombi la serikali la kuhalalisha marufuku hiyo kwa mataifa saba ya waislamu kutoingia nchini Marekani.

Mataifa hayo saba yaliyopigwa marufuku raia wake wasiingine nchini Marekani ni Iran, Iraq, Syria, Yemen, Somalia, Sudan na Libya.

LEAVE A REPLY