Trump ambwaga tena Hillary Clinton kwenye ‘Person of the Year 2016’

0
128

Rais mteule wa Marekani, Donald Trump ameendelea kuhesabu ushindi hata nje ya uchaguzi mkuu wa Marekani baada ya jarida maarufu duniani la Time Magazine kumtaja kama ‘Person of the Year for 2016.

Ushindi huo ambao hata hivyo haukutarajiwa kabisa na kambi yake umekuja kufuatia ushindio wa kushtukiza dhidi ya Hillary Clinton kwenye kinyang’anyiro cha urais wa Marekani.

Trump ameupokea ushindi huo kwa furaha kubwa na amekiambia kituo cha televisheni cha NBC kuwa ‘ushindi huu una maana kubwa sana kwangu’, ‘ni heshima kubwa’

Trump amembwaga tena mpinzani wake, Hillary Clinton na rais wa Urusi, Vladimir Putin.

Ingawa wadau wapenzi wa jarida hilo hushiriki kuchagua mshindi lakini uamuzi wa mwisho hufanywa na wahariri.

LEAVE A REPLY