Trump afanya mazungumzo na Rais wa China kuhusu Korea Kaskazini

0
131

Rais wa Marekani, Donald Trump amefanya mazungumzo na kiongozi wa China Xi Jinping mjini Beijing ambapo yupo kwa ziara maalum.

Trump anatarajiwa kuzungumzia kuhusu vile China inaweza kukabiliana na mipango ya kinyuklia ya Korea Kaskzini swala amblo litatawala ziara yake ya rasi ya Korea.

Marekani inaitaka China ,ambaye ni mshirika mkuu wa Pyongyang kuishinikiza zaidi lakini Beijing imesema kuwa imefanya ya kutosha.

Viongozi hao wa mataifa yenye uwezo mkubwa duniani pia wanatarajiwa kujadiliana kuhusu mapungufu yao ya kibiashara.

Trump aliitaka Korea Kaskazini kuingia mkataba ili kumaliza mipango yake ya utengenezaji wa silaha za kinyuklia, huku pia akiionya dhidi ya uchokozi zaidi dhidi ya Marekani na dunia nzima , akisema ”musitujaribu”.

Pia ameitaka China kufutilia mbali ushirikiano wao na Pyongyang na kusisitiza wito wa Beijing kulishinikiza taifa hilo.

China imesema kuwa inafanya kila iwezalo na kusisitiza kuwa inatekeleza vikwa vya Umoja wa matiafa kwa ukamilifu.

 

LEAVE A REPLY