TRL yabadil ratiba ya usafiri wa Treni nchini

0
335

Kampuni ya reli Tanzania ‘TRL’ imetangaza kubadilishwa kwa muda wa kuondoka treni ya abiria kutoka Dar es salaam kwenda bara kuanzia Agosti 2 mwaka huu ambapo treni itaondoka saa 9 alasiri badala ya saa 11 jioni ilivyozoeleka.

 Mabadiliko hayo yamefanyika ili kutoa nafasi kwa treni ya pili ya huduma ya jiji kutoka kituo kikuu cha reli cha Dar es salaam kwenda Pugu ambayo itaanza kutoa huduma Jumatatu Agosti Mosi mwaka huu.
 Huduma ya treni imeelezwa itakuwa ya awamu mbili asubuhi na alasiri ambapo treni ya kwanza itaondoka kituo cha Pugu saa12 asubuhi na kuwasili kituo cha Dar es salaam saa12:55 asubuhi na kufanya safari 3 zitakazomalizika saa 05:15 asubuhi.
 Jioni pia kutakuwa na safari 3 ambapo treni ya kwanza itaondoka kituo cha Dar es salaam saa 09:55 alasiri kwenda pugu na kuwasili staa10:50 jioni na safari ya mwisho kutoka Pugu kwenda Dar es salaam itakuwa saa 03:20 usiku.

LEAVE A REPLY