TRA yavifunga vituo 710 vya mafuta nchi nzima

0
139

Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imevifungia vituo ya vituo 710 vya mafuta nchi nzima tangu ianze kazi ya kuvikagua vituo hivyo kuona kama vinatumia mashine za kieletroniki za malipo (EFDs).

Vituo 469 kati ya hivyo ndiyo vipo kwenye mchakato wa kufunguliwa baada ya kukidhi vigezo vilivyowekwa na Mamlala hiyo.

Kigezo kingine ni kufunga mashine za (EFPP) kwa wale wote waliokwishanunua, lakini hawakufunga au waliofunga mashine hizo, lakini wakawa hawajaunganisha na pampu zao za mafuta.

Vituo vingine 241 vilivyosalia bado havijafunguliwa kutokana na kushindwa kukidhi masharti ya TRA na makubaliano.

Kwa mujibu wa Kamishna wa Kodi za Ndani wa TRA, Ndg Elijah Mwandumbya, amesema makubaliano hayo ya muda maalumu yanamruhusu mmiliki wa kituo cha mafuta kuendelea kutumia mashine za kawaida mpaka hapo mashine za kisasa zitakapofungwa.

Kamishna Mwandumbya ametoa onyo kali kwa wamiliki wa vituo vya mafuta ambao watashindwa kutekeleza agizo la kufunga mashine za EFDs kwa muda uliowekwa kuwa watachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kufungwa vitu vyao na kufikishwa mahakamani.

 

LEAVE A REPLY