Tozo wodi ya wazazi zaiponza Muhimbili

0
141

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Ummy Mwalimu, ameitaka bodi ya hospitali ya Muhimbili kueleza sababu za kuwalipisha kina mama kinyume na sera ya taifa ya afya.

Mwalimu amesema baada ya kusikia taarifa hiyo, ameutafuta uongozi wa bodi ya hospitali hiyo kwa ajili ya kutaka maelezo na sababu za kutoza fedha hizo.

Amesema utaratibu unaotumiwa na hospitali hiyo ni kinyume cha Sera ya Taifa ya Afya ya mwaka 2007 inayosisitiza kuwa kina mama wajawazito ni lazima wapate huduma hizo bure.

Pia Mwalimu amesema suala hilo wamekuwa wakilisisitiza kila mara na wataendelea kulisisitiza, ili kila hospitali ya umma itoe huduma bure kwa wanawake walio kundi la msamaha.

LEAVE A REPLY