Tongwe Records yafungwa baada ya Roma na wenzake kutekwa

0
480

Mkurugenzi wa Studio ya Tongwe Records, Junior Makame (J-Muder) amesema kuwa studio hiyo kwasasa imefungwa kutokana na mkasa wa kutekwa kwa wanamuziki wakiwa ndani ya studio hizo.

Wasanii waliotekwa ndani ya studio hiyo ni ‘Roma Mkatoliki na wenzake watatu, Moni, Imma na Bin Laden ambapo walipatikana baad ya siki tatu.

J-Murder amesema kuwa kwasasa studio hiyo iliyopo Masaki jijini Dar es imefungwa na haifanyi kazi kwa sasa kutoka na kuwa na hofu ya kutekwa tena.

Pia mkurugenzi huyo amesema kuwa studio hiyo itafunguliwa baada ya mambo yaliyotokea kukaa sawa ndiyo itafanya kazi.

Roma anaendelea kuuguza majeraha huku polisi wakiendelea na uchunguzi kwenye sakata hilo la utekwaji.

LEAVE A REPLY