Tizeba amkosoa meneja wa ranchi ya Ruvu kuhusu vifo vya Ng’ombe 185

0
132

Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk. Charles Tizeba ameikosoa taarifa ya meneja wa ranchi ya Ruvu Dk. James Mtae kuhusu via vya ng’ombe 185 waliofariki kwa ukame mkoani Pwani.

Meneja wa ranchi ya Ruvu, Dk. James Mtae alidai kuwa ranchi hiyo imepoteza ng’ombe zaid ya 180 ambao walifariki kutokana na njaa kati ya kipindi cha mwezi Oktoba na Disemba.

Ng’ombe waliofariki kutokana na ukame unaoukabili ukanda wa Pwani pia wameisababishia hasara ranchi hiyo.

Pia taarifa hiyo iliongeza kuwa mifugo hiyo ilikufa kutokana na kukosa majani katika eneo hilo na ingawa kuna majani yalipelekwa kutoka Kongwa mkoani Dodoma lakini nayo yaliisha na kupelekea kufariki kwa mifugo hiyo.

Hata hivyo taarifa hiyo ya Dk. Mtae imekosolewa na waziri wa mifuko Dk. Charles Tizeba aliyedai kuwa jitihada zilizofanyika kuokoa maisha ya ng’ombe hao hazikuwa toshelezi na kuna uzembe ulifanyika.

LEAVE A REPLY