Tiwa Savage ndani ya Wasafi Festival Dar

0
230

Waandaaji wa Wasafi Festival wametangaza kuwa msanii Tiwa Savage wa Nigeria ni miongoni mwa wasanii watakaotoa burudani kwenye tamasha hilo Novemba 9 mwaka huu.

Msanii huyo anatarajiwa kutoa show kwenye tamasha hilo litakalofanyika katika viwanja vya Posta Kijitonyma Jijini Dar es Salaam siku ya Jumamosi Novemba 9 mwaka huu ambapo ni kwa mara ya kwanza Tamasha hilo linafanyika jijini Dar es Salaam.

Tamasha la Wasafi Festival sasa limefikia jijini Dar es Salaam baada ya kutoa burudani baadhi ya mikoa nchini sasa burudani imeamia jijini Dar es Salaam.

Waandaji wa Tamasha hilo ambao ni WCB chini ya Diamond Platnumz wamesema kuwa tamasha hilo litakusanya wasanii wakubwa wa Afrika hivyo amewataka mashabiki wajitokeze kwa wingi siku ya Novemba 9 mwaka huu katika viwanja hvyo.

Tiwa Savage ataungana na Wizkd pamoja na Innos B kama wasanii kutoka nje ya Tanzania watakao tumbuiza kwenye tamasha hilo la muziki katika jiji la Dar es Salaam.

Tamasha hilo linatarajia kuanza mida saa moja usiku na kumalizika saa sita usiku hivyo mashabiki watapata burudani mbali mbali zikiwemo muziki wa Dansi na Singeli.

LEAVE A REPLY