Timbulo afunguka video yake ya kwanza

0
218

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ally Timbulo maarufu kama Timbulo amesema alipoteza moja ya video yake kutokana na kushindwa kulipa deni la sh.15, 000.

Timbulo alisema ilikuwa ndio video yake ya kwanza kwenye muziki wa bongo fleva, lakini kiasi hicho cha fedha kilimkwamisha kuipata video hiyo.

“Kwanza nilipata changamoto ya kupata fedha ya kutengeneza video hiyo ambayo nilikuwa sijaipa hata jina, nikamuomba mwaandaaji anipe ili baada ya kuingia sokoni niweze kumlipa kwa kuwa ningeweza kupata fedha, lakini alikataa kabisa.

“Nilijua ananitania lakini siku zinalivyozidi kwenda nikawa namtafuta simpati na nikienda studio kwake simkuti hivyo video hiyo ikapotea kwa sababu ya sh.15, 000 tu,” alisema msanii huyo.

LEAVE A REPLY