Timbulo adai hana hofu ya kufungiwa kwa nyimbo zake

0
217

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Timbulo amefunguka na kusema kuwa hana hofu kufungiwa kwa nyimbo kwani muziki wake unazingatia maadili ya kiafrika.

Kauli hiyo ya Timbulo imejiri baada ya wimbi la nyimbo za wasanii nchini kufungiwa kutokana na ukosefu wa maadili.

Timbulo amesema muziki wake una asili ya Kiafrika na siyo asili ya Ulaya kama wanamuziki wengi wanavyofanya ambao wanaacha maungo nyeti wazi au kucheza kihasara hivyo hana hofu kabisa kwamba serikali itamfungia.

Amesema kuwa “Sina muziki wenye asili ya Ulaya, muziki wangu ni wa Kiafrika, kwa hiyo sina shaka na kufungiwa maana hata video zangu nafanya zenye maadili yanayotakiwa ambapo zinaangaliwa na wakubwa kwa wadogo,”

Hata hivyo aliwataka wasanii wenzake kufuata utaratibu kwani kila mahali kuna utaratibu na sheria zake hivyo inawapasa kuzingatia hilo ili kuweza kusonga mbele zaidi.

LEAVE A REPLY