Tiketi za kuhudhuria kuaga mwili wa Nipsey Hussle zamalizika

0
178

Tiketi za kuingia ukumbi wa Staples Center kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Nipsey Husslezimeisha ndani ya dakika chache tu baada ya kuwekwa mtandaoni.

Inaelezwa kuwa mwili wa Nipsey Hussle utaagwa siku ya Alhamis April 11,2019 mjini Los Angeles kwa mujibu wa ratiba iliyoandaliwa na familia ya marehemu taratibu zote zitaanza saa nne asubuhi.

Nipsey alifariki March 31,2019 baada ya kupigwa risasi nje ya duka lake ‘The Marathon Clothing” mjini Los Angeles.

Inaripotiwa kutokana na mchango alioutoa Nipsey kwa jamaii basi eneo la makutano ya barabara mjini Los Angeles litapewa jina la ‘Nipsey Hussle Square’ kama heshima kwa mchango wake mkubwa ikiwa eneo hilo linaloziunganisha barabara za Slauson Avenue na Crenshaw BlvdNipsey.

LEAVE A REPLY