TID atangaza kuwania ubunge jimbo la Kinondoni uchaguzi wa mwaka 2020

0
171

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Khalid Mohamed (T.I.D) ametangaza nia ya kuwania ubunge katika jimbo la Kinondoni kwenye uchaguzi ujao mwaka 2020.

TID ambaye ameachana na matumizi ya dawa za kulevya amesema kuwa sababu inayomsukuma kugombea nafasi hiyo ni kutokana na mbunge wa sasa Maulid Mtulia kushindwa kulitimizia mahitaji ya wananchi katika jimbo hilo.

Kutokana na mbunge huyo kushindwa kutimiza kazi zake kama mbunge, TID ameamua kutumia nafasi hiyo kuhakikisha anamng’oa ifikapo 2020.

TID amesema kuwa yeye anafahamu vizuri matatizo yanayowakabili wakazi wa Kinondoni kutokana na kuwa mzaliwa wa mahali hapo.

Pia  TID amesema iwapo atapewa dhamana ya kuliongoza jimbo hilo, atahakikisha anatatua matatizo yote yanayowakabili watu wa Kinondoni, likiwemo janga la madawa ya kulevya ambapo limekuwa kubwa sana.

Lakini TID ajasema atagombea jimbo hilo kupitia Chama gani ila amewaka nia ya kugombea kwenye uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2020.

LEAVE A REPLY