TID atupilia mbali kejeli dhidi yake

0
49
TID

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, T.I.D ametupilia mbali maneno ya kejeli ya wasanii wenzake wanapomiwta kuwa yeye ni mtoto wa mama kwa sababu tu amekuwa akiishi nyumbani kwa mama yake na hataki kuahama hapo.

Kauli ya mwanamuziki imekuja baada ya watu kusema kuwa mwanamuziki huyo ni mtoto wa mama kwasababu toka awe maarufu bado anaishi na mama yake maeneo ya Kinondoni jijini Dar es Salaam hivyo watu wanamchukulia kama mtoto wa mama tu.

Hata hivyo msanii huyo ameonekana kutokujali swala hilo na kusema kuwa hata watu wanaokaa na kujaji swala hilo  Hawana cha maana wanachomiliki zaidi ya maneno katika mitandao ya kijamii.

Amesema kuwa mimi sijali pale mtu anaponiita mtoto wa mama kama yeye mwenyewe anatembea kwa miguu na wengine wanalala getto, wachafu, wananuka mdomo hivyo siwezi kuwasemea.

T.I.D akiwa kama moja ya wasanii wakongwe, anasema  kuwa amekuwa na shida ya kutapekiwa pesa zake na platform za muziki kwa kuwa wao wanauza muziki wake na wanashindwa kumlipa.

LEAVE A REPLY