TID anataka kutumia skendo ya ‘unga’ kupata collabo na Diamond Platnumz?

0
647

Baada ya kuwa msanii mtegemewa katika kutoa habari za mastaa wanaotumia dawa za kulevya badala ya kuwa staa wa muziki, Khalid Mohamed a.k.a TID sasa anatafuta namna ya kurudi zaidi kwenye sanaa.

Staa huyo ambaye ameachia ngoma yake mpya ya MAISHA ya JELA iliyorekodiwa mwaka 2007 baada ya kukaa rumande kwa siku 4 sasa ana mpango wa kufanya kazi na Diamond Platnumz.

Staa huyo amewaeleza mashabiki wake kuwa tayari ameshafikisha ombi la ufanya kazi na Dangote na tayari ameshawasilisha IDEA ya ngoma na vitu vingine vya msingi.

TID anataka kutumia skendo ya unga kupata collabo alizozitamani muda mrefu?

Diamond Platnumz alikuwepo siku zote na TID alikuwa akifanya mambo yake…..lakini kwakuwa kwa sasa media zimeanza kumuangazia kwa send iliyomkuta huenda akatumia ‘fursa’.

LEAVE A REPLY