TID akataa kuitwa jina la ‘Mnyama’

0
87

Mwanamuziki wa Bongo Fleva Khaleed Mohamed maarufu kama Top in Dar ‘TID’ ameibuka na kuweka wazi kuwa kuanzia sasa hataki kutumia jina la Mnyama kwasababu kila mtu anatumia jina hilo.

Kauli ya mwanamuziki huyo imekuja baada ya baadhi ya wanamuziki kutaka kujiita jina hilo ambaye yeye aliamua kujiita.

Kama utakumbuka siku za nyuma moja ya majina ya TID ilikuwa ni jina la Mnyama Lakini TID aliingia kwenye mgogoro na baadhi ya wasanii huku kisa kikiwa ni jina hilo.

TID amewahi kugombania jina na Diamond Platnumz ambaye alikuwa anajiita simba Lakini pia aligombania jina na Dudubaya ambaye anajiita Mamba Lakini pia aligombania jina Mr. Blue.

Lakini hatimaye TID kaweka siku zake za kugombania jina nyuma yake kwani ametangaza Kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa kuanzia Hivi sasa hataki hata kulisikia jina hilo.

Kuanzia sasa mwanamuziki huyo amesema kuwa hataki kusikia mtu yoyote anamwita jina hilo kwasababu hataki matatizo na wasanii wenzake ambao wanapenda kutumia jina hilo.

LEAVE A REPLY