TID afunguka tofauti yake na Q Chilla

0
20

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, TID amekiri kusema huko nyuma walipoteza vipaji vingi, muda mwingi na nguvu kazi kutokana na vitu ambavyo havikuangaliwa mbali.

TID amefunguka hilo wakati anasimulia anachokikumbuka kwenye tofauti yake na msanii Q Chief wakati walipokuwa kwenye bendi moja ya Top Band ila baadaye alifuatwa na polisi kwa madai ya haki miliki ya wimbo wa nilikataa.

TID amesema kuwa “Q Chief ndiyo aliniambia anataka kujiunga Top Band kwa sababu kabla ya hapo bendi ilikuwepo na ilikuwa inafanya kazi kama kawaida.

Pia amesema kuwa kuhusiana na wimbo wa nilikataa ulikuwa mkubwa tukauza na Album lakini Q Chief akaja na mapolisi kunidai pesa na kusema hataki maendeleo na kazi ya Top Band kwa hiyo nimlipe chake aende”.

Mwisho amemalizia kwa kusema kuwa “Ilikuwa ni kitu cha kijinga sana naona tulipoteza vipaji vingi, muda mwingi na nguvu kazi ya kutosha kwa sababu ya kitu ambacho hakikuangaliwa kwa umbali,  nikampa milioni  2 kutokana mauzo ya Album kisha nikamwambia aondoke asigeuke nyuma”.

LEAVE A REPLY