Thomas Ulimwengu kuibeba Yanga?

0
327

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania na timu ya soka ya TP Mazembe ya Congo, Thomas Ulimwengu huenda akaifanyia ‘ihsani’ timu ya Yanga ya Dar es Salaam kwa kuisaidia TP Mazembe kuifunga MO Bejaia muda mfupi ujao.

Timu hizo zinazokutana kwenye mchezo wa marudiano wa kundi A unatarajia kuanza majira ya saa 10:30 (GMT +3) kwenye uwanja wa TP Mazembe jijini Lubumbashi nchini Congo.

Ushindi kwenye mechi hiyo mbali ya kuipa matumaini timu ya Yanga ya kuweza kufuzu kwa hatua ya nusu fainali lakini pia utaihakikishia TP Mazembe nafasi ya kucheza hatua hiyo muhimu.

Yanga ya Tanzania inategemea ushindi wa TP Mazembe kwenye mechi mechi mbili ikiwemo ya leo jioni na ile ya TP Mazembe dhidi ya Medeama huku wao wakiwa na jukumu la kushinda mechi mbili zilizobaki ikiwemo mechi ya marudiano ugenini dhidi ya TP Mazembe.

Hata hivyo Thomas Ulimwengu hatoweza kuonyesha uzalendo kwa timu ya nchi yake kwakuwa sheria za michezo ya vilabu haziruhusu wachezaji kufanya upendeleo wa kusaidia matokeo ya kuzibeba timu zisizo zao.

Ulimwengu anatarajia kuanza mechi ya leo na kuwa nguzo muhimu ya ushambuliaji kwa mabingwa hao wa zamani wa ligi ya mabingwa Afrika.

LEAVE A REPLY