The Undertaker aachana na Mieleka

0
40

Mchezaji mielekea Mark William Calaway maarufu The Undertaker amethibitisha rasmi kujiuzulu kutoka World Wrestling Entertainment (WWE) baada ya miaka 30.

The Undertaker aliingia ulingoni katika mchezo wa mwisho wa Survivor Series Novemba 22 2020 usiku, ambapo aliuhutubia umma wa mashabiki wa WWE Universe kwa mara ya mwisho.

Wakati wa hotuba yake, Undertaker alieleza ni kwanini ameamua kujiuzulu.

“Kwa miaka 30 nimekuwa nikiingia ndani ya ulingo huu taratibu na kuwaangusha watu mara kwa mara,” alisema.

“Sasa wangu muda umefika. Muda wangu umefika wa kumuacha Undertaker apumzike… kwa … amani,”.

The Undertaker anajiuzulu akiwa ndiye mchezaji bora wa WWE kuwahi kushuhudiwa katika mashindano hayo na amekuwa ulingoni kwa miongo mitatu.

LEAVE A REPLY