Tetesi za usjaili barani Ulaya, Ozil aitamani Manchester United

0
128

Kiungo wa Arsenal, Mesut Ozil amesema kuwa angependa kuhamia Manchester United badala ya Barcelona ikiwa ataondoka Arsenal.

Wakala wa Ozil ameimbia Barcelona kuwa ni lazima wafanye uamuzi ikiwa watamsaini mchezaji huyo au la katika kipindi cha wiki mbili zinazokuja.

Nahodha wa Barcelona Andres Iniesta anasema mshambuliaji wa Liverpool Philippe Coutinho, 25, atakuwa muhimu ikiwa watamuendea mwezi Januari.

Ronaldo anawaomba ushauri mawakili wake kujaribu kuondoka Real Madrid. (El Chiringuito kupitia Daily Express)

Willian amewahakikishia mashabiki wa Chelsea kwamba hataondoka mwezi Januari, baada mchezaji huyo wa safu ya kati kuhusishwa na kuelekea huko Manchester United na Barcelona.

Newcastle wanatathmini kumpa ofa mshambuliaji wa Liverpool Danny Ings, 25 na mlinzi wa Manchester United Luke Shaw, 22, mwezi ujao.

Jose Mourinho amemuorodhesha mchezaji wa safu ya kati wa Inter Milan raia wa Ureno Joao Mario, 24, kama atakayechukua mahala pake Henrikh Mkhitaryan huko Manchester United.

Kipa wa AC Milan Gianluigi Donnarumma, 18, ametaka mkataba wake mpya kufutwa huko Real Madrid wakati Paris St-Germain wakitaka kumsaini.

Sporting Lisbon wanataka kumchukua mshambuliaji wa Leicester Islam Slimani, 29, kutoka Ureno kwa mkopo mwezi Januari.

LEAVE A REPLY