Tetesi za usajili Ulaya, Man U yahamishia nguvu kwa Rose wa Tottenham

0
158

Manchester United wana hofu kuwa meneja Jose Mourinho anaweza kujiuzulu mwishoni mwa msimu.

Mourinho ana matumaini ya kuishawishi bodi ya Mancheter United kutoa dola milioni 50 kwa ofa ya kumsaini beki wa Tottenham Danny Rose.

Inter Milan wana mpango wa kumsaini kiungo wa kati wa Manchester United Juan Mata ambaye mkataba wake unafikia mwisho msimu huu.

Liverpool wanatarajiwa kufanya mazungumzo leo Alhamisi kuhusu kuhama kwa Philippe Coutinho kwenda Barcelona huku fedha za kuhama kwake zikitarajiwa kuwa euro milioni 50.

Liverpool wametambua kiungo wa kati wa Monaco Thomas Lemar, 22, kama mtu atakayechukua mahala pake Coutinho.

Tottenham wanataka kumfanya Harry Kane, 24, kuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi katika ligi ya primia kwa kumlipa pauni 200,000 kwa wiki.

Bayern Munich wamethibitisha kutaka kumsaini kiungo wa kati ya Schalke Leon Goretzka, 22, ambaye awali aliwavutia Liverpool.

Kiungo wa kati wa Liverpool Emre Can, 23, hataondoka Januari na yuko katika mazungumzo ya mkataba mpya na klabu hiyo licha ya Juventus kuonyesha nia ya kumsaini.

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola, anataka kutumia pauni milioni 50 kuboresha kikosi chake huku Alexis Sanchez, 29 na mlinzi wa Real Sociedad Inigo Martinez, 26, wote wakilengwa.

LEAVE A REPLY