Tetesi za usajili Ulaya, Man U kumsajili Danny Rose

0
371

Mshambuliajia wa Manchester City, Raheem Sterling, 22, atasitisha mazungumnzo kuhusu mkataba mpya huko Etihad hadi baada ya kombe la dunia.

Mshambuliaji wa Chelsea na Ubelgiji Eden Hazard anaendelea na mkataba mpya pauni 300,000 kwa wiki huko Stamford Bridge kwa matumaini ya kuwavutia Real Madrid.

Mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez anasema kuwa mchezaji mwenzake wa zamani Neymar, ambaye kwa sasa yuko huko Paris St-Germain hawezi kujiunga na Real Madrid.

Arsenal wana nia ya kumuuza Theo Walcott, 28, mwezi Januari huku klabu yake ya zamani ya Southampton na West Hama wakimzea mate wing’a huyo wa England.

Nyota wa zamani wa Juventus Alessandro del Piero, anaamini mchezaji wa safu ya kati wa Liverpool mjerumani Emre Can, 23, atakuwa bora zaidi katika klabu hiyo ya Italia.

Mancheseter United wana uhakika kuwa watamsaini mlinzi wa Tottenham na England Danny Rose, 27, kwa pauni milioni 50 aidha mwezi Januari ua msimu ujao.

Haki miliki ya picha Getty Images Image caption Rafael Benitez

Meneja wa New Castle Rafael Benitez anataka paunia milioni 20 mwezi Januari kuweza kuwanunua wachezaji watatu.

West Ham watakabiliwa na ushindani kutoka Real Madrid kusaini Fyodor Smolov, 27, mshambuliaji wa Krasnodar na Urusi.

Real Madrid watajaribu kumsaini kipa wa Bilbao Kepa Arrizabalaga, 23, na mshambuliaji wa Inter Milan Mauro Icardi, 24, mwezi Januari.

.

 

LEAVE A REPLY