Tetesi za usajili barani Ulaya, Chelsea wamtaka Danny Rose wa Tottenham

0
370

Baada ya kuanza vibaya kwenye mechi ya kwanza ya ligi kuu nchini Uingereza, klabu ya Chelsea wanajiandaa kutoa pauni milioni 50 kumsajili beki wa Tottenham Danny Rose.

Tottenham wamefikia makubaliano na PSG kumsajili beki Serge Aurier ambaye alikuwa akifuatiliwa na Manchester United.

Tottenham wana uhakika wa kukamilisha usajili wa beki wa kati wa Ajax, Davinson Sanchez, 21, kwa pauni milioni 27.

Dau la Chelsea la kumtaka beki Alex Sandro, 26, limekataliwa na Juventus.

Meneja wa Chelsea anataka Alex Sandro awasilishe maombi ya kuondoka Juventus baada ya dau la pauni milioni 52 na 61 kukataliwa

Kiungo wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain anataka pauni 150,000 kwa wiki ili kujiunga na Chelsea.

Chelsea wanajaribu kumsajili mshambuliaji wa Torino Andrea Belotti, 23, kuziba nafasi ya Diego Costa.

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amesema klabu yake itakataa dau lolote la kumtaka Alexis Sanchez, 28, na Alex Oxlade-Chamberlain, na anatarajia wawili hao kuheshimu mikataba yao.

Liverpool wanataka kiungo Ivan Rakitic, aunganishwe kwenye mkataba wa Barcelona kumsajili Philippe Coutinho.

Real Madrid wapo tayari kuwazidi kete Tottenham na kumsajili beki wa Ajax Davinson Sanchez.

Manchester City sasa wamemgeukia Eden Hazard wa Chelsea baada ya kubadili mawazo ya kumtaka Alexis Sanchez.

 

LEAVE A REPLY