Tetesi za Usajili barani Ulaya, Coutinho kutua Barcelona Januari hii

0
294

Kuna uwezekano mkubwa kwamba Liverpool watamruhusu Philippe Coutinho, 25, kuhamia Barcelona mwezi huu wa Januari kwa £140m.

Klabu ya Chelsea wanamtaka meneja wa Atletico Madrid, Diego Simeone achukue nafasi ya Antonio Conte katika klabu hiyo mwisho wa msimu.

Chelsea wamezidisha juhudi zao za kutaka kumnunua kiungo wa kati wa Everton na England Ross Barkley, 24, na pia wameulizia kuhusu uwezekano wa kumnunua mshambuliaji wa England na West Ham Andy Carroll, 28.

Mchezaji wa Celtic na Scotland Kieran Tierney, 20, amejumuishwa katika orodha ya mabeki wa kushoto ambao Manchester United wanawatafuta kuimarisha safu yao ya ulinzi, pamoja na kinda wa Fulham Ryan Sessegnon, 17.

Paris St Germain wanatarajiwa kutoa ushindani kwa Tottenham katika kutafuta saini ya Sessegnon ambaye thamani yake imekadiriwa kuwa £30m.

Juventus wana imani kwamba watafanikiwa kumchukua Emre Can kutoka Liverpool bila kulipa ada yoyote mwisho wa msimu.

Klabu hiyo ya Serie A imemuahidi mchezaji huyo wa miaka 23 mshahara wa £85,000 kwa wiki.

Manchester United wameanzisha mazungumzo ya kuongeza mikataba ya wachezaji wane kwa mwaka mmoja. Wachezaji hao ni viungo wa kati wa Uhispania Juan Mata, 29, na Ander Herrera, 28, beki wa England Ashley Young, 32, na beki Mholanzi Daley Blind, 27.

Manchester United wanataka sana kumnunua beki wa kushoto wa Juventus Sandro lakini wanavunjwa moyo na Juve kutotaka kumuuza mchezaji huyo wa miaka 26.

Tottenham wanatarajiwa kutoa mikataba mipya yenye donge nono zaidi kwa mshambuliaji wa England Harry Kane, 24, na beki wa Ubelgiji Toby Alderweireld, 28.

Marseille wanamnyatia kiungo wa kati wa Arsenal Jack Wilshere lakini mchezaji huyo wa miaka 26 anataka kusalia na Gunners.

Mkufunzi mkuu wa Monaco Leonardo Jardim amesema hana nia ya kumuuza mshambuliaji wake Mfaransa Thomas Lemar, 22, kwa Liverpool mwezi huu.

Meneja wa Paris St-Germain Unai Emery amefungua mlango kwa winga wa Brazil Lucas Moura, 25, na mwenzake wa Ufaransa Hatem Ben Arfa, 30, kuihama klabu hiyo Januari.

Mbelgiji Thibaut Courtois, 25, anakaribia kutia saini mkataba mpya Chelsea baada ya klabu hiyo kumpa ujira wa zaidi ya £200,000 kwa wiki, hatua itakayomfanya kuwa kipa anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani.

Beki wa Chelsea David Luiz, 30, anataka sana kuondoka klabu hiyo na anatumaini Real Madrid watamtaka.

Mkufunzi mkuu wa Newcastle Rafa Benitez anatafakari uwezekano wa kutaka kumnunua nahodha wa Watford Troy Deeney.

LEAVE A REPLY