Tetesi za usajili barabi Ulaya leo Juni 17

0
333

Real Madrid imesema mshambuliaji wake Cristiano Ronaldo hajaiambia klabu hiyo kuwa anataka kuondoka (ABC).

Hata hivyo, mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ureno hajapanga kurejea Spain baada ya kucheza katika Kombe la Shirikisho linalofanyika Urusi (Record).

Ronaldo alimuwambia wakala wake Jorge Mendes miezi miwili iliyopita kuwa anataka kuondoka Madrid (AS).

Chelsea hawapo tayari kumpa mamlaka makubwa Antonio Conte kwenye suala la usajili, huku kukiwa na tetesi kuwa meneja huyo anazidi kughadhabishwa na kutokuwepo na usajili wowote (Guardian).

Lakini Chelsea wamesisitiza kuwa hawana mpango wowote wa kumuachilia Conte aondoke na watampa kila msaada katika suala la usajili, huku mikataba ya wachezaji wanne ikiandaliwa ukiwemo wa Romelu Lukaku, 23, na kitita cha usajili huenda kikafikia pauni milioni 250 (Daily Mirror).

Manchester City wamemkabidhi Pep Guardiola pauni milioni 300 kwa ajili ya usajili, lakini City hawataki kulipa pauni milioni 70 kumnunua beki wa kati wa Southampton Virgil van Dijk, 25 (Manchester Evening News).

Arsenal wameripotiwa kupanda dau la kuvunja rekodi ya dunia la zaidi ya pauni milioni 100 pamoja na Olivier Giroud ili kumsajili Kylian Mbappe kutoka Monaco (Sun).

Chelsea hawana mpango wa kumruhusu Conte aondoke, na watamkabidhi pauni milioni 250 za usajili kuthibitisha hilo (Mirror).

Manchester United watamsajili winga Ivan Perisic kwa pauni milioni 44 wiki chache zijazo (Mail).

David de Gea ameongeza juhudi za kutafuta nyumba Spain wakati akijiandaa kuondoka Manchester United (Star).

Michy Batshuayi atakataa kwenda West Ham, huku akijaribu kujadili na Chelsea mustakbali wake (Express).

Kipa wa AC Milan Gianluigi Donnarumma amependekezwa kwenda Manchester United na wakala wake Mino Raiola (Diario Gol).

Manchester United na Liverpool watalazimika kutoa pauni milioni 50 iwapo wanataka kumsajili kipa wa Leicester City Kasper Schmeichel (The Sun).

Beki wa kati wa Roma Kostas Manolas anasakwa na Chelsea kwa pauni milioni 42 (Sport FM 94.6 ya Ugiriki).

Manchester United na Juventus zitamfuatilia kiungo wa Barcelona Andre Gomes (AS).

Klabu yoyote inayotaka kumsajili Cristiano Ronaldo kutoka Real Madrid italazimika kutoa euro milioni 400 (Gazzetta dello Sport).

Kiungo wa Monaco Tiemoue Bakayoko amechagua kujiunga na Chelsea na kuzitosa Manchester City na Manchester United (L’Eqipe).

Bayern Munich bado wanamfuatilia kiungo wa Paris Saint Germain Marco Verratti, licha ya kumsajili Corentin Tolisso kutoka Lyon (Bild).

Kipa wa akiba wa Manchester City Willy Caballero, 35, anatarajiwa kuthibitishwa kuwa usajili wa kwanza wa Chelsea wa msimu (Evening Standard).

Tottenham wamewaambia Manchester United kuwa watalazimika kutoa pauni milioni 50 kumsajili kiungo Eric Dier, 23 (Daily Telegraph).

Arsenal watarejea tena Lyon wakiwa wameongeza dau kufikia karibu pauni milioni 50 kutaka kumsajili Alexandre Lacazette, 26. Dau la awali la pauni milioni 30 lilikataliwa msimu uliopita (Daily Telegraph).

Lyon wapo katika mazungumzo ya kina ya kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Chelsea Bertrand Traore, ambaye alikuwa Ajax kwa mkopo msimu uliopita (Evening Standard).

Beki wa kulia wa Juventus Dani Alves ameshutumiwa vikali na mashabiki kwa kusema Pablo Dybala, 23, anatakiwa kuondoka Juve iwapo anataka kupata maendeleo katika soka (Il Giornale).

Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal na Manchester United Robin van Persie, 33, anakaribia kuondoka Fenerbahce na kwenda Feyneerd ya Uholanzi (FR12.nl).

West Ham wanataka kumsajili winga wa Middlesbrough Adama Traore, 21, lakini Middlesbrough wamesema hawana tatizo la fedha (Teeside Gazette).

Inter Milan watataka pauni milioni 45 kutoka kwa Manchester United wanaotaka kumsajili winga Ivan Perisic, lakini United wanataka kutoa Pauni milioni 30 (Manchester Evening News).

Kiungo mshambuliaji wa Bayern Munich Douglas Costa, 26, anakaribia kuhamia Juventus kwa kitita cha pauni milioni 26, ambapo amekubali mkataba wa miaka mine (L’Equipe).

Arsenal wanatarajiwa kuwazidi kete Everton katika kumsajili mshambuliaji wa AC Milan M’Baye Niang, 22, ambaye alikuwa Watford kwa mkopo msimu uliopita (Hertfordshire Mercury).

Birmingham bado wanasubiri jibu kutoka kwa nahodha wa zamani wa Chelsea John Terry, 36, ambaye amekubali dau lao la pauni 100,000 kwa wiki (Daily Mirror).

Swansea bado wanazungumza na Galatasaray kuhusu kuwauzia Bafetimbi Gomis, 31, ambaye alikuwa Marseille kwa mkopo msimu uliopita (Wales Online).

Hull na Newcastle zote zinamuania mshambuliaji wa Chelsea Tammy Abraham, 19 kwa mkopo (Sun).

LEAVE A REPLY