Ted Cruz ‘amkaushia’ Donald Trump

0
143

Mashabiki na wanachama wanaomuunga mkono mgombea urais wa marekani kwa tiketi ya Republican, Donald Trump usiku wa kuamkia leo wamemzomea kwa fujo gavana wa jimbo la Texas, Seneta Ted Cruz baada ya seneta huyo kukataa katakata kumuunga mkono hadharani mgombea urais huyo.

Seneta Ted Cruz alikuwa akitoa hotuba kwenye mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika kwenye jimbo la Cleveland nchini Marekani.

Wakati akikaribia kuhitimisha hotuba yake Seneta, Cruz hakuonekana kujali kutomuunga mkono Trump hali iliyoanza kuzua makelele ya chini chini kabla ya wafuasi wanaomuunga mkono Trump kudhihirisha hasira zao kwa kupaza sauti kubwa na kumtaka Cruz atangaze kumuunga mkono Trump aliyekuwa mpinzani wake mkubwa kwenye kinyang’anyiro cha mchujo kwenye kura za maoni siku za nyuma.

Kwenye hotuba yake, Seneta Cruz alimpongeza Trump kwa kuchaguliwa kwake na chama hicho kuwa mgombea urais bila ya kutaja neno lolote la kumuunga mkono.

Donald Trump na Seneta Cruz wanadaiwa kuwa na tofauti za kimitazamo pamoja tofauti binafsi zinazodaiwa kuanzishwa na Trump kwa kumdharau baba mzazi wa Seneta Cruz, Rafael Cruz alipohoji iwapo Rafael Cruz anahusika na mauaji ya aliyekuwa rais wa Marekani John Kenedy wakati wa kampeni za mchujo wa kuwa za maoni.

Inadhaniwa kuwa Seneta Cruz aliichukulia siku ya jana kama nafasi pekee ya kulipiza kisasi kwa kumdhalilisha Trump.

Mahasimu?: Donald Trump na Ted Cruz
Mahasimu?: Donald Trump na Ted Cruz

LEAVE A REPLY