Taylor Swift na Kim Kardashian wazidisha uhasama kuhusu ‘Famous’

0
381
Taylor Swift & Kim Kardashian: Nani anazungumza ukweli?

Utata unaoletwa na ngoma mpya ya Kanye West ‘Famous’ umezidi kuwa mkubwa baada ya mke wa staa huyo Kim Kardashian kuamua kuweka kwenye mtandao wa Instagram na Snapshot video kadhaa zikimuonyesha West akifanya mazungumzo na sauti ya kike inayodhaniwa kuwa ya Taylor Swift.

Kwenye video hiyo West anaonekana akikubaliana na sauti hiyo atumie mistari tata juu ya msanii Taylor Swift, lakini Taylor Swift aliyeongoza kwa kupata mkwanja mrefu zaidi mwaka jana amekanusha kufikia makubaliano na Kanye West.

Baada ya Kim kuachia video hizo na kudai kuwa Swift anaudanganya umma kuwa hakufahamu mistari itakayoimbwa na West dhidi yake kwenye wimbo huo, Taylor Swift amemtaka Kim kuonyesha (kama anayo) video ambayo West alimsikilizisha kipande cha mistari ‘tata’ ambayo inamdhalilisha staa huyo.

Swift anadai aliwasiliana na West kuhusu nyimbo hiyo na walikubaliana kuwa West amsikilizishe mistari ambayo yeye (Taylor) ameimbwa vibaya lakini West hakuwahi kumsikilizisha hadi alipokuja kuisikia baada ya nyimbo kuachiwa rasmi.

Stunt? Kanye West na Taylor Swift
Stunt? Kanye West na Taylor Swift

LEAVE A REPLY