Tanzia: Mwanamuziki Shaban Dede wa Msondo Ngoma afariki dunia leo

0
660

Mwanamuziki mkongwe nchini kutoka bendi ya Msondo Ngoma, Shaaban Dede amefariki dunia leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa amelezwa kwa matibabu.

Mtoto wa marehemu, Hamad Dede amesema kuwa baba yake alilazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili akipatiwa matibabu kwa zaidi ya wiki mbili.

Pia amesema kuwa msiba upo nyumbani kwa marehemu Mbagala na anatarajiwa kuzikwa huku huko nyumbani kwake Mbagala jijini Dar es Salaam.

Wakati wa uhai wake Marehemu, Shabani Dede aliwahi kuimba katika bendi mbali mbali kama vile Tabora Jazz, Bima Lee, Mlimani Park, Msando Ngoma ambako alikuwa akifanya kazi ya muziki hadi umauti kumkuta leo.

Mpaka umauti unamkuta leo mwanamuziki huyo alikuwa anaimba katika bendi ya Msondo Ngoma Music Band baada ya kujiunga nayo mwaka 2011 akitokea bendi ya Sikinde ambao ni wapinzani wakubwa wa Msondo Ngoma.

LEAVE A REPLY