Tanzia: Godzillah afariki dunia

0
201

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Godzilla amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumatano majira ya saa 10 alfajiri nyumbani kwao salasala jijini Dar Es Salaam.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo, iliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam na msiba upo nyumbani kwao Salasala.

Taarifa za awali zimedai kuwa kabla ya kufika na umauti, Godzilla alikuwa akusumbuliwa na tumbo  pamona na kisukari.

Godzilla aliwahi kutamba na nyimbo kama vile Get High, King Zilla, Milele aliyomshirikisha Alikiba, First Class na aliyomshirikisha Mwasiti, Stay na nyingine kibao.

LEAVE A REPLY