Tanzia: Aliyekuwa mume wa Irene Uwoya, Ndikama afariki dunia

0
257

Aliyekuwa mume wa muigizaji wa filamu nchini, Irene Uwoya, Hamad Ndikumana amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.

Chanzo cha kifo chake kinasemekana ni matatizo ya moyo ambapo jana alikuwa akiendelea na kazi zake kama kawaida.

Mpaka anakutwa na umauti Ndikumana alikuwa kocha msaidizi wa kikosi cha Rayon Sports ya Rwanda.

Alikuja nchini mara ya mwisho wakati wa Simba Day Agosti 8, akitua nchini Agosti 7 akiwa na kikosi cha Rayon ambacho kilicheza na Simba na kupoteza kwa bao 1-0.

Alizaliwa Oktoba 5, 1978 na mpaka anafariki dunia alikuwa ametengana na Uwoya kwa mingi na alikuwa ndiye mkewe waliyefunga naye ndoa katika Kanisa Katoliki na walibahatika kupata mtoto mmoja  ambaye jina lake ni Krish.

LEAVE A REPLY