Tanzania ‘hoi’ michuano ya gofu Afrika Mashariki

0
97

Mabingwa watetezi wa mashindano ya East Africa Challenge Cup Golf timu ya taifa ya Uganda imefanikiwa kutetea taji lake kwa kufungana pointi na timu ya taifa ya Kenya.

Uganda ambayo sasa inakuwa bingwa wa michuano hiyo kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kulitwaa nyumbani jijini Kampala mwaka 2014 kisha kurudia ushindi huo jijini Kigali Rwanda imefanikiwa kulitwaa taji hilo kwa mara nyingine jijini Addis Ababa.

Uganda na Kenya zilifungana kwa kupata pointi 16 baada ya kumalizika kwa mzungumko wa mwisho mwishoni mwa wiki.

Kwenye mashindano hayo timu ya taifa ya Tanzania iliambulia nafasi ya nne ikiwa na jumla ya pointi 11 huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Kenya kutokana na sheria za michuano hiyo.

Nafasi ya tatu ilienda kwa Ethiopia huku Tanzania ikiburuza mkia.

Sheria za mchezo huo kwa nchi za Afrika Mashariki zinaurudisha ubingwa kwa bingwa mtetezi iwapo itatokea kufungana pointi kileleni kati ya bingwa mtetezi na mshindani mwingine.

LEAVE A REPLY