Tanesco: Shoti iliyomuondoa Mramba yawakuta na wengine wanne

0
240

Hali ya Uongozi ndani ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) imeendelea kwenda kombo baada ya wakurugenzi wengine watatu kupigwa ‘STOP’ huku mkurugenzi wa rasilimali watu Watson Mwakyusa akijipa ‘red card’ mwenyewe.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya shirika hilo ambayo gazeti za Mtanzania iliipata kisha kuthibitishwa na Kaimu Mkurugenzi mpya Dk. Tito Mwinuka ni kuwa wakurugenzi Declan Mhaiki aliyekuwa Naibu Mkurugenzi Mtendaji (Usambazaji umeme) Mhandisi Sophia Mgonja aliyekuwa Naibu Mkurugenzi Mtendaji (Uzalishaji na Huduma kwa Mteja), na Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uzalishaji Umeme, Nazir Kachwamba wameshushwa vyeo.

Wakati hao wakibadilishiwa majukumu aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali Watu, Watson Mwakyusa ameandika barua ya kuacha kazi kwa manufaa ya umma.

Inadaiw akuwa wakurugenzi walioshushwa vyeo wamehamishiwa katika Chuo cha Mafunzo cha Tanesco (TSS).

Siku ya Jumapili Rais Dk. John Magufuli alitengua uteuzi wa aliyekuwa bosi wa shirika hilo Mhandisi Felchesmi Mramba kufuatia sakata la kupandishwa kwa bei ya umeme.

LEAVE A REPLY