Tanasha atangaza ujio wa EP yake

0
128

Mpenzi wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz aitwae Tanasha Donna amefunguka na kusema kuwa anatarajia kuachia EP yake ‘Donatella’ hivi karibuni.

Kwa mujibu wa taarifa yake ya awali kupitia ukurasa wake wa Instagram kuhusu hilo, Tanasha alithibitisha kuwa uzinduzi wa EP yake hiyo utafanyika Januari 31, 2020.

Mbali na kutajwa kwa tarehe hiyo ya uzinduzi huo, Diamond Platnumz alithibitisha kuwa Uzinduzi utafanyika mjini Nairobi nchini Kenya kwenye ratiba yake ambapo ilionekana kuwa atahudhuria uzinduzi huo.

Tanasha ambaye ni raia wa Kenya amesema kuwa kwenye EP yake hiyo imefanywa kwa hali ya hivyo mashabiki wa muziki wake wake mkao wa kula kwa ajili ya kupokea EP hiyo.

Tanasha ameongeza kwa kusema kuwa kwenye EP yake amepata mchango mkubwa kutoka kwa mpenzi wake Diamond Platnumz.

LEAVE A REPLY