Tanasha apinga kumtumia Diamond kupata umaarufu

0
41

Mwanamuziki kutoka nchini Kenya, Tanasha Donah amejibu madai ya kumtumia staa wa muziki Diamond kujipatia umaarufu katika muziki wake.

Tanasha amesema kuwa “Sijamtumia Diamond ili kupata umaarufu kwani hapo mwanzo nilikuwa napinga kuyaanika mahusiano yetu kwa uma”.

Tanasha ameongeza kuwa “Nilimpenda sana hata yeye mwenyewe anajua kuwa nilimpenda. Alikuwa na uwezo wa kuchukua simu yangu na kuikagua na hata yeye mwenyewe alikuwa anasema mimi ni muaminifu”

Mwisho amesema kuwa alimpenda na ataendelea kumpenda Diamond kama baba wa mtoto wake lakini hawezi kumtumia kujipatia umaarufu wake.

LEAVE A REPLY